30
Uganda kama nchi mwanachama mojawapo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inalo jukumu la kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili. Katiba …
Uganda kama nchi mwanachama mojawapo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inalo jukumu la kuendeleza na kukuza lugha ya Kiswahili.
Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inapendekeza Kiswahili kama lugha ya mawasiliano ya kikanda. Aidha, katiba ya nchi ya Uganda ya 1995 iliyofanyiwa marekebisho mnamo mwaka 2005 pamoja na hati maalumu ya serikali "The government white paper" ya 1992; zinatoa matamko bayana kuhusu uendelezaji wa Kiswahili nchini Uganda.
Kwa hivyo, Wizara ya Elimu na Michezo kupitia Kituo cha Taifa cha Ukuzaji Mitaala, ilifanya mabadiliko katika mtaala wa elimu kwa kiwango cha sekondari ya daraja la chini na kusisitiza mafunzo ya lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kimeandikwa kulingana na silabasi ya mtaala mpya ambao unasisitiza shughuli za mafunzo kwa ajili ya kumpa mwanafunzi umilisi pamoja na kukuza stadi za kimaisha na maadili katika kila mada husika. Katika kitabu hiki, kila mada kuu imegawanywa katika mafunzo mbalimbali. Mafunzo hayo pia yamehusisha shughuli kadhaa.
Katika kila funzo, stadi za lugha kama vile, Kusikiliza, Kuzungumza, Kusoma na Kuandika, zimesisitizwa. Kwa hivyo, ili kupata umilisi wa stadi lengwa kutokana na kila mada, mwanafunzi anatakikana kusoma maelekezo na kushiriki katika kufanya shughuli zote za kila mada husika.

Shughuli za mafunzo, zitampa mwanafunzi fursa ya kufanya utafiti na kujigundulia maarifa kuhusu masuala kadhaa hasa yanayozungumziwa katika silabasi. Mwanafunzi anatakiwa kufanya utafiti kwa kutumia mtandao wa intaneti, kamusi, maktaba, magazeti, majarida au kwa njia yoyote nyingine. Aidha, kuna uwezekano kwamba, mwanafunzi ataweza kufanya shughuli za mafunzo kwa kutumia ujuzi pamoja na tajriba aliyonayo kutokana na mazingira yake.
Shughuli za mafunzo kadhaa zinahimiza ushirikiano kupitia vikundi. Kwa hivyo, mwanafunzi atajifunza zaidi kutokana na wenzake wakiwa Katika vikundi darasani. Kutokana na mijadala yao, wataweza kuwa na uwezo wa kushughulikia vipengele mbalimbali vya shughuli za mafunzo bila ugumu wowote.

Course Currilcum
- Mada kuu 4.1: Uzalendo Details FREE 1 year
- Mada kuu 4.2: Amani na Usalam Details FREE 1 year
- Mada kuu 4.3: Migogoro na Maridhiano Details FREE 1 year
- Mada kuu 4.4: Jinsia Details FREE 1 year
- Mada kuu 4.5: Ngoma na Burudani Details FREE 1 year
- Mada kuu 4.6: Magonjwa Details FREE 1 year
- Mada kuu 4.7: Rasilimali Details FREE 1 year



